News
Loading...

Hata John Terry akipatikana na hatia atatozwa faini ya pauni 2500 tu za kiingereza!


Imebainika kuwa kesi ya ubaguzi wa rangi inayomkabiri John Terry haina uzito kama magazeti na vyombo vya habari vya nchi hiyo vinavyolikuza suala hilo. Sheria ya nchi hiyo inasema kuwa mtu akipatikana na hatia ya kutumia lugha ya kibaguzi dhidi mwingine adhabu yake ni faini kiduchu ya pauni 2500. Kesi ya John Terry imekuwa ikikuzwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo kiasi kwamba utafikiri kuwa endapo akipatikana na hatia huenda akafungwa japo miezi miwili la la hasha ni faini ndogo tu ambayo kwa mtu kama John Terry anaweza akailipa hiyo na akwauliza kama wangependa awaongeze mara kumi ya hizo 2500. Nafikiri imefika wakati serikali ya Uingereza ikaiangalia tena hiyo adhabu kama ni sahihi ama la, vinginevyo tutaendelea kusika vitendo na kauli za kabaguzi vikiendelea hata katika karne hii ya 21. Na si England pekee yenye adhabu kiduchu kwa kosa hilo, aliyekuwa kocha mkuu wa Spain Luis Aragones aliwahi kutozwa faini ya pauni 2000 tu na UEFA baada ya kutoa kauli baguzi dhidi ya Thierry Henry. Kazi ipo katika mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi "LETS KEEP FIGHTING TO ERADICATE RACISM"

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :