News
Loading...

Serikali ilikuwa wapi, wananchi hawa wakijenga huku mabondeni?


Maeneo ya jangwani karibu na klabu ya Yanga.
Kila yanapotokea mafuriko katika maeneo haya huwa najiuliza serikali ilikuwa wapi wananchi hawa walipoanza kujenga misingi, kuta na hatimae kuezeka. Jana unamsikia mkuu wa mkoa anawaambia jamani hameni huku hapafai, sasa wao kama serikali walikuwa wapi kuwavunjia mara walipoanza ujenzi? Au ndio walikuwa wanatishiwa kunyimwa kura? Mbona pale SEA VIEW na PALM BEACH walivunja mara moja? Unaweza ukajionea mwenyewe jinsi serikali za nchi hii zinavyofanya kazi, na unajiuliza labda waliwaacha wajenge ili itakapofikia kuvunjiwa waongeze sifuri na kujilia mapesa ya mlipa kodi. Kwa sababu haiingii akilini kuwa serikali haikujua kuwa jangwani hapafai na kuwazuia watu kujenga katika maeneo hayo. Na yote hayo ni faida ya kuendesha kila suala kisiasa. Nafikiri umefika muda hawa mabwana wa kijani kibichi wapumzishwe, kwani wamefanya kazi kwa miaka mingi na wamechoka wanahitaji msaada!

Haya hayajawahi kuwa maeneo slama watu kuishi.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :