News
Loading...

Ama kweli nyani Mourinho haoni bado lake!Jose Mourinho kocha wa Chelsea FC na mshambuliaji wa timu hiyo Samuel Eto'o chini
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amejikuta akikukamilisha msemo wa Nyani haoni kundule pale aliporekodiwa akiwaponda washambuliaji wake na chaneli ya Tv Canal plus ya Ufaransa. Mourinho aliyekuwa akisubiri kuhojiwa na chaneli hiyo alikuwa akiongea na mfanya biashara wa Ki
Swizi alirekodiwa akimwambia "Tatizo la Chelsea sina washambuliaji" kisha akaongeza "Nina Eto'o lakini ana miaka 32" Au pengine 35 nani ajuae? Canal plus bila kufanya ajizi wakarusha hewani kauli yake hiyo pale timu yake inapojiandaa na mchezo muhimu dhidi ya Galatasaray utakaochezwa kesho nchini Uturuki, jambo liliompelekea Mourinho kukasirika na kudai Canal plus hawana weledi wa kazi waliporekodi mazungumzo binafsi na kuyarusha hewani.

Kwa maoni yangu tu Mourinho hapaswi kuzungumzia weledi pale ambapo yeye mwenyewe ni bingwa wa choko choko hasa kwa makocha na wachezaji wa vilabu vingine, siku hiyo hiyo alirekodiwa pia akimzungumzia Radamel Falcao ambaye ni mshmbuliaji wa klabu Monaco alikaririwa akisema "Falcao anahitaji timu na Chelsea inahitaji Mshambuliaji, akaongeza mchezaji kama yeye hawezi kucheza mbele ya watazamaji 3000 tu" akimaanisha Monaco haina watazamaji wengi kitu ambacho bila shaka viongozi na washabiki wa Monaco watakerwa sana na kauli hiyo. Hivyo basi Jose Mourinho aache kulalama "He
should get on with it" kama Waingereza wasemavyo!
habari na picha kwa hisani ya dailystar

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :