News
Loading...

Kamanda Barlow ulikuwa wapi?



Liberatus Barlow
Kamanda wa polisi Tabora

















Katika gazeti la habari leo la leo kuna taarifa isomekayo
Disko toto marufuku Krismasi, Mwaka Mpya Tabora.

Sababu zilizotelewa na Kamada wa Polisi mkoani Tabora Bw Liberatus Barlow,
ni kuwa bado tuna machungu na vifo vya watoto wetu 19 waliokufa kutokana na kukosa hewa katika ukumbi wa Bubles mwaka 2008. Ni kweli vifo vile bado vibichi mioyoni mwetu sote. Mungu awalaze mahali pema vijana wetu hawa.

Cha ajabu tu ni kauli hii kuchukua takriban miaka miwili na nusu hivi tangu tukio. Najiuliza sipati jibu. Pia ninavofahamu pahala palipohusika na tukio lile (NSSF) palipigwa marufuku kupigwa disco tangu wakati wa tukio na hapatumiki tena. Sasa hili katazo hili jipya hata sielewi linalenga nini hasa.

Lakini napenda kumpongeza Kamanda Barlow kwa angalau kuruhusu toto Disco
kupigwa katika kumbi za wazi kwa kipindi hicho cha sikukuu za krismasi na mwaka mpya, japo na watoto nao wapate pa kwenda wafurahie siku kuu kama wenzao wa Dar na kwingineko Tanzania. Nasema hivi kwa kuwa mwaka fulani palikuwa na maadhimisho ya Mwl J.K. Nyerere, Tabora ilikuwa marufuku kupiga muziki hata katika baa, wachilia mbali disco na dansi. Lakini sasa mikoa mingine yote iliendelea na starehe kama kawaida. Jijini Dar es Salaam Fm Academia katika show yao siku hiyo walibandika picha kubwa ya hayati Mwalimu, hiyo yote ilikuwa ni kuadhimisha kifo chake si kuomboleza.

Siku hiyo wenye kumbi za starehe Mjini Tabora wakakosa kuingiza pesa na TRA ikakosa makusanyo kwa siku hiyo, sasa huku kama si kujirudisha nyuma ni nini? Mkoa wenyewe uliachwa nyuma tangu baada ya uhuru.

Viongozi wa Tabora amkeni na muyakumbatie maendeleo na si kukumbatia ulofa,majungu na fitna ndio maana huo mkoa unaishia kupewa ahadi zisizotekelezwa pamoja na kuwa ndio ulichangia ushindi mnono kwa CCM na katika uchaguzi mkuu 2010  na harakati za kupigania uhuru miaka ya 1950 kwa kiasi kikubwa lakini hauthaminiwi kwa kuwa nyie viongozi wa Tabora hamuuthamini mkoa huo.

Kwanza wekeni vitanda 20 zaidi wodi ya wazazi Kitete na mambo mengine yafuate. Ni aibu sana eti Hospitali ya rufaa ya mkoa ina vitanda kumi tu katika wodi ya wazazi kiasi kwamba wanalazwa wawili mpaka watatu katika kitanda kimoja.

Naongea yote haya kwa kuwa mimi ni mwana Tabora wa damu kabisa hivyo najua ninachokiongea na nyie mnajua najua.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :