Bw Tido Mhando |
Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa TanzaniaJ.K Kikwete |
Tarehe 17/12/2010 gazeti moja liliandika kuhusu kutemwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika la utangazaji la Tanzania TBC Bw Dustan Tido Mhando baada ya serikali kuamua kutoongeza mkataba wake, ambapo kwa mujibu wa Tido serikali ilipaswa kiutaratibu imfahamishe miezi sita iliyopita kuwa haina mpango wa kusaini tena mkataba na yeye, ili ajipange. Hilo halikufanywa.
Kwa mtu yeyote mwenye akili tamimu utajiuliza kulikoni serikali kuvunja taratibu za uajiri huku wakijua wafanyacho si sahihi? Ndipo inapokuja dhana kwamba Tido kupitia TBC alikuwa mkweli na muwazi sana hasa katika mchakato wa kuelekea uchaguzi mkuu 2010 kuliko ambavyo muajiri wake angependa awe. Na kibaya zaidi kwa Bw Tido, Chama kikongwe kilipoteza viti vingi tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe nchini mwaka 1992. Lawama hizo anabebeshwa yeye. Hivyo basi kaka Tido aelewe kosa lake kwa aliyekuwa mwajiri wake ingawa si kosa kwa wale wasiofungamana na upande wowote.
Na hili la Tido si jipya, kwani tumelishuhudia likitokea katika kinyang'anyiro cha kugombea uspika kwa tiketi ya Chama kikongwe kwa kaka Sitta kuenguliwa katika nafasi ya kugombea uspika. Na sababu ni zile zile kuwa spika aliyepita alifuata zaidi kanuni za Bunge kuliko kuangalia maslahi ya chama kikongwe ambacho yeye ni mwanachama wake. Sababu zilizotolewa eti kuwapa nafasi wanawake nao washike mhimili mmoja kati ya mitatu katika uendeshaji wa nchi. Jamani mkianza kutoa vyeo kama zawadi tutafika kweli?
|
Mh Samuel Sitta |
Mwisho kabisa tulichojifunza kutokana na haya matukio ni kuwa Chama kikongwe, viongozi wake na wa serikali hawajakomaa kidemokrasia na hawako tayari kuwepo na upinzani thabiti, hivyo basi sasa tutegemee kupotea kwa uhuru wa TBC kwa yeyote atakayepewa nafasi hiyo kumrithi Tido Mhando anakuwa ameshaonywa kupitia alichofanyiwa Bw Tido. Tumekwisha!
0 comments :
Post a Comment