News
Loading...

Mgawa jezi nani Simba?Kikosi cha Simba Sports Club
na chini ni kikosi cha Yanga

Gazeti moja la michezo leo limeripoti kuwa uongozi wa klabu ya Simba kuwa umempa jezi nambari tisa Ally Shiboli
ambaye amesajiliwa katika dirisha dogo la usajili kutoka KMKM ya Zanzibar na Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi Godfrey Nyange (Kaburu) alithibitisha hilo kutokea.

Kinachonishangaza mimi ni vipi uongozi wa Simba ukajihusisha na ugawaji wa jezi kwa wachezaji? kwa mtazamo wangu mimi hiyo ilikuwa kazi ya kocha  Patrick Phiri kwa kuwa ndiye anayewajua wachezaji wake kwani ni yeye ndiye atakuwa alipendekeza kwa uongozi Shiboli asajiliwe katika dirisha dogo la usajili. Napenda kuwaasa viongozi wa klabu za Simba na Yanga kuacha tabia ya kuingilia kazi za makocha, wajenge tamaduni za kisasa ambapo kule Man United hutomsikia CEO David Gill anazungumzia jezi na namba zake kama ambavyo hutomsikia Sir Allex Ferguson akizungumzia vifungu vya mkataba wa klabu hiyo na AON. Na si dhambi yeye Sir Allex kuzumgumzia hilo, ila huo ni mgawanyo wa madaraka tu na unaheshimiwa na pande zote husika. Kwa leo ni hayo tu, na sasa tujipange vema na michezo migumu inayokuja dhidi ya TP Mazembe toka DRC kwa upande wa Simba na Haras el Hodoud dhidi ya Yanga. Klabu hizo kongwe nchini zitacheza dhidi ya timu hizo za DRC na Egypt kama zitafanikiwa kuvuka raundi ya kwanza ambapo zitapambana na timu nyepesi toka Comoro na Ethiopia.FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :