News
Loading...

Mh Anne Makinda aliweza au aliwezeshwa?


Mh Anne Makinda
Spika wa Bunge la Jamuhuri
 ya muungano wa Tanzania
Mh Samuel Sitta
Spika mstaafishwa

Kuna swali najiuliza kila siku Je? kitendo cha NEC/CCM kuamua kukata majina ya wagombea wanaume wote waliojitokeza kugombea uspika wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho kikongwe kilikuwa ni kizuri kwa wanawake na harakati zao za kutaka usawa katika ngazi za kufanya maamuzi? Kwa sababu kilichofanywa pale ni kuwa wanawake waliwezeshwa si kuwa waliweza wenyewe, ili kuweza Mh Anne Makinda alipaswa kushinda mwenyewe tangu mwanzo wa mchakato hadi pale katika fainali ambapo napo angepambana na wagombea wa kiume na akawashinda, hapo ningesema kaweza mwenyewe. Lakini utaratibu mzima uliotumika kupata mgombea uspika kwa tiketi ya CCM unatia mashaka mno, Huhitaji kuwa hata umesoma mpaka darasa la saba kulitambua hilo. Pia wanawake nchini Tanzania wanapaswa wajue kuwa kuna tofauti kati kuweza na kuwezeshwa.

Inaelekea wazi kuwa  NEC/CCM ilidhamiria kumuondoa Samuel Sitta katika kinyang'anyiro hicho cha uspika kwa kuhofia huenda angeshinda na kurudi tena katika nafasi hiyo na huenda angeendelea kutenda haki bungeni, pamoja na kuwa utendaji wake katika bunge lililopita ulikaribia kusababisha avuliwe uanachama kule Kizota Dodoma. Huu ni mtazamo wangu mimi mbumbumbu mzungu wa reli.


Hili ndilo jengo la Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :