News
Loading...

Kaseja 1 Maximo 0Juma Kaseja

Juma Kaseja kaudhihirishia umma wa wa Tanzania kuwa kocha wa zamani wa Taifa stars Marcio Maximo alikuwa akimbania kwa kutomuita katika timu hiyo kwa zaidi ya miaka mitatu mfululizo aliyoifundisha timu hiyo kwa kile alichoeleza kuwa Kaseja hakuwa na nidhamu ndio maana aliamua kutomwita katika vikosi vyake vya Stars bila kuueleza umma wa Tanzania Kaseja alimkosea nini. Hata alipobanwa na vyombo vya habari kadha wa kadha aeleze ni utovu gani wa nidhamu ambao haukustahili kusamehewa Maximo aligoma kueleza pamoja na Kaseja mwenyewe kuomba msamaha mara kadhaa kupitia vyombo vya habari, Maximo aliweka pamba mbichi masikioni. Mungu si Athumani baada ya Maximo kuondoka na Mdenmark Jan Paulsen kurithi kazi ya kuifundisha Taifa Stars, bila hiana kocha huyo kutoka Denmark alimuita Kaseja katika timu yake ya kwanza kuichagua. Kwa bahati mbaya Kaseja akavunjika kidole akiwa mazoezini na Stars wakati ikijiandaa kucheza na Algeria na kumsababishia kukosa mechi hiyo dhidi ya Algeria iliyochezwa nje kidogo ya jiji la Algiers ambapo Shaban Kado aliikaimu nafasi hiyo vizuri mno pamoja na kuwa mwamuzi wa mchezo huo alikuwa mbaya kwa stars bado tulifanikiwa kutoka sare ya bao moja kwa moja na Algeria nchini kwao.

Hata hivyo Juma Kaseja alirejea langoni mwa Stars siku ilipocheza na kufungwa goli moja kwa sifuri na timu nzuri na yenye uzoefu ya Morocco iliyomjumuisha mshambuliaji Marouane Chamakh wa Arsenal ya Uingereza.

Marco Maximo


Jan Poulsen
Ivo Mapunda
Pia Kaseja akacheza michezo yote katika mashindano ya CECAFA Tusker Challenge 2010 kuanzia ile ya makundi mapaka ule wa fainali ambapo alifanikiwa kuzuia penelti moja iliyoisadia Kili Stars kubeba kombe hilo. Mpaka hapo nafikiri Kaseja pia amemuumbua Marcio Maximo, ambaye mafanikio pekee aliyoipatia stars ni kushiriki CHAN nchini Ivory Coast mwaka 2009. Ambako tuliishia raundi ya kwanza tukiwa na pointi nne baada ya matokeo ya kufungwa mchezo mmoja, sare moja na kushinda moja. Maximo ambaye katika juhudi zake za kutaka kulifuta kabisa jina la Kaseja midomoni mwa washabiki wa soka hapa nchini aliwatumia makipa kadhaa bila mafanikio nao ni pamoja na Ivo Mapunda, Shaban Dihile, Mwarami Hamis pamoja na makipa wa akiba namba mbili na namba tatu wa Simba Sports Club, Ally Mustapha na Deo Mushi(Dida).

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :