News
Loading...

Kuna tofauti kati ya serikali ya Tanzania na Arsene Wenger?


Wachezaji wa Man United wakishangilia bao la kwanza.
Mh Mrisho Kikwete, Rais wa Tanzania.
Sidhani kama utajiuliza juu ya jibu la swali hilo hapo juu, jibu ni hakuna, wawili hao yaani serikali ya Tanzania na Arsene Wenger wote hawawajali watu waliowatuma wawafanyie kazi nao ni wa Tanzania na wapenzi na mashabiki wa The Gunners! Nikianza na Serikali ya Tanzania 1. Imeendelea kuwanunulia mawaziri na manaibu wao, na wakuu wa mikoa na wa wilaya magari ya kifahari wakati hali za huduma za kijamii nchini haziridhishi. Na huduma hizo ni kama kwa mfano tu Hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete haina vitanda vya kutosha katika wodi ya wazazi, ina vitanda 10 na vinahitajika 30 ! Na kwa upande wa Arsene Wenger 1.Hataki kununua wachezaji wenye hadhi ya kimataifa ili kuwaongezea nguvu wale watoto wenye vipaji  vya hali ya juu, pamoja na kuwa hiyo ni kero ambayo washabiki wa Arsenal wamekuwa wakiilalamika tangu aondoke Thiery Henry na wenziwe ambao waliifanya Man united kufanya kazi ya ziada kupata sare mechi dhidi yao wachilia mbali kushinda. Hapa nimetaja chache tu zipo nyingi hasa katika serikali ya Tanzania. Haya yote yamekuja baada ya Man utd kuidhalilisha Arsenal kwa kuifunga goli 2-0 dimbani Oldtrafford  katika mashindano ya kombe la FA huku United wakitumia wachezaji watoto na wale wa akiba. 
Maudhi: Wenger na Galas

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :