Si UEFA tu hata FIFA na English FA ni madikteta wakubwa pia, refa wao akifanya madudu ni sawa lakini ukiongelea madudu hayo umekosea na wanakufungia mechi mbili usikae katika benchi la ufundi, tumeyaona kwa Arsene Wenger na Sir Alex Ferguson wiki tu iliyopita. Yule wa dunia nae anazungumzia watu wenye nafasi kubwa hawapaswi kutoa kauli fulani kwa kuwa watu wa chini wataiga. Lakini yeye atoe kauli zozote hata kama zinawadhlilisha viongozi wa chama cha soka cha nchi fulani. Au hata akidhihaki watu wa jinsia fulani, iwe sawa. Nafikiri Sepp Blatter hapaswi kuzungumzia mchezaji mmoja mmoja akiwa kama rais wa FIFA aviachie vyama husika Dikteta huyu kwa kuwa ana cheo kikubwa sana, haiyumkiniki Mhadhiri wa chuo kikuu abishane na mwanafunzi wa shule ya msingi.
0 comments :
Post a Comment