Hii ni barabara ya Ulaya iliyopo maeneo ya Cheyo Tabora. |
Katika maunganiko ya barabara ya Ulaya na barabara inayoelekea Chuo cha ardhi, Cheyo mjini Tabora pamewekwa alama ya kuonesha mchepuko wa kuingia kulia ili kupisha ujenzi wa barabara ya Kilimatinde unaoendelea kwa kiwango cha lami (bila shaka) tatizo lililopo hapa ni kuwa alama za mchepuko zimewekwa hapo hapo ulipo mchepuko na kana kwamba hilo halitoshi alama nazo ni ndogo mno na zimewekwa nje ya barabara kana kwamba hazina umuhimu kwa mtumiaji wa barabara hiyo. Kwani si rahisi kuziona hasa ukiwa katika mwendo wa wastani wa km 40 kwa saa ni lazima utazipita. Ni matarajio yetu baada ya wahusika kusoma makala haya watarekebisha tatizo hili dogo lakini lenye usumbufu na upotevu wa muda kwa mtumia barabara.
Ili kupusha usumbufu kwa mtumia barabara japo wangeweka alama kubwa kama hizi katikati ya barabara ili mtumiajia asisumbuke kwenda mpaka yalipo maunganiko ya barabara ya Kilimatinde na kukuta barabara imefungwa hivyo kumlazimu kurudi tena alipotokea. |
Alama kiduchu ya mchepuko inaoneka kulia mwa barabara |
Hii ndio barabara ya Kilimatinde inayotengenezwa kwa kiwango cha lami |
Ujenzi unaendelea |
Picha na habari kwa hisani ya Aloyce Mlawa wa Aloyson.com
0 comments :
Post a Comment