Ndege iliyoua wachezaji 23 wa Man United mwaka 1958
Giggs akiashiria hajawasikia vema
Katika mchezo wa Carling cup katika uwanja wa Elland road Mashabiki wa timu za Leeds united na Man united juzi waliendeleza chuki baina yao baada ya mashabiki wa Leeds kuimba nyimbo za kudhihaki vifo vya wachezaji 23 wa Man united vilivyotokea baada ya ndege yao kuanguka mjini Munich mara baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa wa ulaya mwaka 1958 na wale wa Man united kujibu dhihaka hizo kwa kuimba vifo vya mashabiki wa Leeds waliouawa mika 11 iliyopita mjini Istanbul, Uturuki katika fujo zilizotokea kabla ya mchezo kati ya Galatasaray na Leeds united. Tabia hizo zisizo za kistaarabu zinachunguzwa na Polisi wa Yorkshire huko Leeds. Hali hiyo inaonesha jinsi gani timu hizo zilivyo na uhasama usiokwisha pamoja na kuwa Leeds sasa ipo katika ligi daraja la kwanza.
0 comments :
Post a Comment