News
Loading...

Bastola yamponza Rage Igunga!


Mh Aden Rageh akiwa katika mkutano wa hadhara Igunga.


WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, amewaagiza polisi kumhoji Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, kuhusu hatua yake ya kupanda jukwaani na bastola kiunoni. Taarifa iliyopatikana na kuthibitishwa na viongozi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ambao hawakupenda kutajwa, ilisema polisi wameagizwa kuwa baada ya kumhoji mbunge huyo, wawasilishe ripoti hiyo kwake haraka iwezekanavyo. 

Miongoni mwa mambo ambayo polisi wameelekezwa kumhoji Rage ni pamoja na endapo anaimiliki bastola hiyo kihalali. Mambo mengine ni sababu alizoeleza wakati anaiomba bastola hiyo na hatua yake ya kwenda nayo kwenye mkutano wa hadhara.

“Tunasubiri taarifa, tumewaagiza polisi wamhoji. Tunataka kujua mambo matatu; kama silaha hiyo anaimiliki kihalali, pili madhumuni aliyoiombea na tatu kwenda nayo kwenye public meeting (mkutano wa hadhara) wakati kuna watoto, wanawake na watu wa aina mbalimbali,” kilisema chanzo chetu cha habari kikimnukuu Nahodha na kuongeza: “Haiwezekani kwenda na silaha tena nje nje kwenye mkutano kama ule. Sasa tunasubiri taarifa ya polisi.”


Habari na picha kwa hisani ya gazeti la Mwananchi!FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :