News
Loading...

Benki kubwa nchini yachukua zaidi ya saa 1 kumpatia 15M mteja wake!


Hii ndio gari iliyotuweka benki zaidi ya saa nzima
Siku ya alhamisi nilimsindikiza mjomba wangu benki kutoa shilingi 15 milioni toka kwa akaunti yake, ili anunue gari. Baada ya kufika katika tawi la benki hiyo maarufu lililopo maeneo ya Mikocheni karibu na ITV ambalo pia huwa na wateja wachache wanaofika hapo kwa mahitaji yao, ilimchukua mjomba wangu dakika 5 kujaza fomu ya kutolea pesa na tano nyingine kufika dirishani. Dirishani hapo alitakiwa aende katika dawati la huduma kwa wateja ambako aliambiwa asubiri wafanye uhakiki na tawi lake lililopo mjini karibu na mgahawa wa Steers. Mjomba akaja kukaa na mimi tukisubiri, baada ya dakika 15 mjomba alienda kuuliza kama uhakiki ulishafanyika akajibiwa bado, hatimae tukajikuta tumekaa benki hapo kwa muda usiopungua dakika 50 bila mafanikio yeyote. Ndipo nikasema lazima niwaulize na mimi kulikoni? Wakanijibu kuwa majibu hayajarudi ndipo nikawawashia moto wa kistaarabu na kuwaambia kuwa mimi si mteja wa benki hiyo lakini kwa mfano waliouonyesha siku hiyo sina hata hamu ya kufikiria nifungue akaunti nao. Baada ya kelele zangu na kudai kumuona meneja wakatupatia pesa within 10 minutes. Kumbe inawezekana!


Maoni yangu
Kuwa watumishi wa benki hiyo hawakujali muda wa mteja, sote tunafahamu njia nyingi za kiteknolojia ambazo wangeweza kuzitumia kuhakiki umiliki wa akaunti nikitaja chache ni pamoja na Faksi, baruapepe na hata simu ya mkononi. Kwa kuwa hawapo pale kumhudumia mteja bali bali wapo pale kutimiza mwezi ili wapate mishahara!

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :