News
Loading...

Hawa vipi na maeneo ya wazi?


Hili ndilo jengo linalodaiwa kuwa ni la Mtendaji wa
kata,ambalo limejengwa mbele ya nyumba nyingine
ambazo zipo hapo kisheria yaani viwanja vyake
vimepimwa na wizara ya ardhi.Mbele ya jengo hilo kuna kuta fupi ina rangi ya
kijani na imeandikwa kwa rangi ya njano kwa
bahati mbaya hausomeki vizuri, lakini inasomeka
kama chama cha.................. hata sioni vema.

Hapa ni maeneo ya Kinondoni Msisiri katika barabara ya Dunga, hili ni eneo la wazi lakini hapa pamejengwa jengo zuri tu, inasemekana eti no ofisi ya mtendaji wa kata. Hata kama ni ofisi ya mtendaji wa kata bado hakuna kinachompa mamalaka ya kuvamia sehemu ya wazi na kujenga hasa kama eneo lenyewe lina nyumba nyingine ambazo jengo hilo linalodaiwa ni la mtendaji wa kata linaziziba. Napenda kumuomba Mh Anne Tibaijuka afike na huku kwani maeneo mengi ya wazi yamevamiwa na taasisi zinazojiita nyeti lakini hazionyeshi unyeti wao kwa kufuata sheria na taratibu bali kwa kuzivunja na kuzipinda ili kukidhi mahitaji yao.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

1 comments :

Anonymous said...

hicho ni chama cha mapinduzi.