News
Loading...

Ukosefu wa vitanda hospitali Tabora


Mh Aden Rageh-
Mbunge Tabora Mjini
Mara nyingi tumekuwa tukisoma magazetini jinsi watu flani wakivichangia vyama vya siasa mamilioni ya shilingi halali za ki Tanzania ama kwa ajili ya kampeni au kwa matumizi mengine tu. Je katika hali kama tuliyoiona jana usiku kupitia kituo cha Runinga cha taifa TBC1 kina mama waja wazito kulala wawili mpaka watatu katika kitanda kimoja cha futi tatu tu, wafadhili hawa hawaoni wakiisaidia wodi ya wazazi katika hospitali ya Kitete mkoani Tabora watakuwa wamefanya jambo la maana sana si tu kwa chama kimoja cha siasa bali kwa wananchi wote wa Tanzania? Mimi nawaomba wale wote wenye uwezo tujitahidi kuchangia ama kwa pesa taslimu au kwa wale wenye kuweza kununua vitanda hivyo, wawasiliane na kampuni itengenezayo vitanda hivyo kupitia tovuti yao kama inavyoonekana hapa; made-in-china.com

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :