|
Mh Bw Zitto Kabwe |
|
Bw Wilbrod Slaa-Katibu mkuu
Chadema |
Tangu baadhi ya wabunge wa Chadema watoke nje ya bunge baada ya Mh Rais Kikwete aanze kulihutubia bunge hilo kwa mara ya kwanza tangu liapishwe rasmi, ndani ya Chadema kumekuwa kukifukuta kichinichini. Lakini katika wiki za karibuni tumeshuhudia mbunge kijana machachari Bw Kabwe Zitto alivuliwa unaibu kiongozi wa upinzani bungeni, pia tumesoma kuwa Bw Kabwe Zitto akisema hatambui kuvuliwa uongozi wowote. Pia tumesoma kuwa Bw Kabwe Zitto ametishia kujiuzuru nafasi zote za uongozi alizo nazo pamoja na ubunge ambapo akajibiwa na Dr Slaa kuwa Chadema itaendelea kuwepo hata wakiondoka yeye Dr Slaa pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Bw Freeman Mbowe, hivyo awe na amani na maamuzi yeyote atakayoyaamua juu ya vyeo vyake ndani ya Chadema. Ni msimamo mzuri na thabiti kuutoa hasa suala lenyewe likiwa linajdiliwa katika vyombo vya habari. Katka malumbano unachopaswa kufanya ni kutoa majibu mazito zaidi ya mlumbana mwenza. Nashangaa kwamba Chadema na busara zao zote hawaoni suala hili litawapeleka vibaya? Na ingekuwa vema wakayajadili haya
behind the closed doors, au wanataka kuwa kama mcheza mpira anayecheza na jukwaa akishangiliwa anaongeza chenga huku timu yake ikiwa imeshafugwa goli 2-0?
FACEBOOK COMMENT
Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
.
0 comments :
Post a Comment