News
Loading...

Inasikitisha sanaHawa ni naadhi ya kina mama wlioipa ushindi mnono CCM mkoani
Tabora leo hii wodi ya wazazi katika hospitali ya Kitete ina vitanda 10 tu, na
inalaza wazazi 30 kwa siku,hali inayopelekea walale wawili mpaka watatu katka kila kitanda


Mh Rais J.Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni
mkoaniTabora
   


   Alhamisi tarehe 16/12/2010 TBC1 habari ya saa 2 usiku imeripoti na kuonyesha picha za video kuwa Hospitali ya mkoa wa Tabora, Kitete General Hospital katika wodi ya wazazi yenye uwezo wa kuhudumia waja wazito 10 kwa wakati mmoja lakini leo hii ina waja wazito 30 na hivyo kupelekea waja wazito hao kulala wawili mpaka watatu katika kitanda kitanda kimoja, hivi kweli vitanda 20 vina gharama kuliko Land Cruiser moja ya waziri au naibu waziri? Na ukisema sana utaambiwa serikali haina pesa, This is too much to take to be honest, tena basi karaha hii wanaipata kinamama wa Tabora ambao katika uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani wa mwaka 2010 walihakikisha wanakirudisha chama cha mapinduzi madarakani kwa kishindo. Kwani mkoani humo wapinzani waliambulia viti viwili tu tena vya udiwani.Kwa kweli hali hii inaudhi na inasikitisha sana. Natoa wito kwa Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Jakaya M. Kikwete, chonde chonde Baba ondoa hii kero ni aibu kwa serikali yako.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Bebedores do Gondufo said...

Very good.

malwasaidi said...

tujitahidi kudai maendeleo ya Tabora huko ndiko viongozi wengi wamesoma, nashindwa kuelewa ni kwa nini wamepasahau.

Anonymous said...

Uchangiaji nao una asili/tabia yake kwanza inabidi tuaanze kwenye familia kuaanda watu tangu wakiwa wadogo wajuwe kuwa kuna kujitolea kwenye jamii kwa ajili ya wengine.
Kassembo