Kwa mara nyingine tena tumeshuhudia kiongozi wa ki Afrika aking'ang'nia madaraka mara baada ya kushindwa katika uchaguzi uliokuwa huru na wa haki, kwa bahati nzuri hata Umoja wa Afrika(AU) wamemtaka aachie madaraka jambo ambalo si aghalabu kutokea hasa pale AU ilipomtetea Comrade Robert Mugabe pamoja na kuwa alishindwa na uchaguzi haukuwa huru na wa haki bado walimtetea abaki madarakani. Vema. Bw Gbagbo ameendelea kupata vikwazo toka kila pande za dunia. Hivi juzi tu Umoja wa Ulaya (EU) kupitia mawaziri wake wa mambo ya nje wamekubaliana kumzuilia visa yeye na wote wanaomuunga mkono kiongozi huyo mbabe na mwenye sapoti kubwa toka kwa jeshi la nchi hiyo. Kama kuzuiliwa visa haitoshi pia mali zake na za washirika wake zitazuiliwa pia. Nchi hiyo imeigia mgogoroni kufatia uchaguzi wa Rais, tume ya uchaguzi ilimtangaza kiongozi wa upinzani Alassane Quattara kama mshindi, lakini Bw Laurent Gbagbo anayevihimili majeshi na vyombo vya habari vya taifa hilo akaamua kung'ang'na madarakani. Kwa upande mwingine Bw Quattara ameshateua baraza lake la mawaziri na anafanyia kazi zake za urais katika hoteli moja mjini Abidjan, amechukua ofisi ya meneja wa hoteli imekuwa ndio ofisi ya Rais. Haya yote ni matokeo ya uchu wa madaraka na ubinafsi miongoni mwa viongozi wa nchi za ki Afrika. Eeh Mungu Ibariki Afrika iondokane na viongozi kama Gbagbo, na ibariki Tanzania tusije tokewa na balaa la kupatakiongozi kama Laurent Gbagbo.
0 comments :
Post a Comment