Hawa ni naadhi ya kina mama wlioipa ushindi mnono CCM mkoani Tabora leo hii wodi ya wazazi katika hospitali ya Kitete ina vitanda 10 tu, na inalaza wazazi 30 kwa siku,hali inayopelekea walale wawili mpaka watatu katka kila kitanda |
Mh Rais J.Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni mkoaniTabora |
Alhamisi tarehe 16/12/2010 TBC1 habari ya saa 2 usiku imeripoti na kuonyesha picha za video kuwa Hospitali ya mkoa wa Tabora, Kitete General Hospital katika wodi ya wazazi yenye uwezo wa kuhudumia waja wazito 10 kwa wakati mmoja lakini leo hii ina waja wazito 30 na hivyo kupelekea waja wazito hao kulala wawili mpaka watatu katika kitanda kitanda kimoja, hivi kweli vitanda 20 vina gharama kuliko Land Cruiser moja ya waziri au naibu waziri? Na ukisema sana utaambiwa serikali haina pesa, This is too much to take to be honest, tena basi karaha hii wanaipata kinamama wa Tabora ambao katika uchaguzi mkuu wa rais,wabunge na madiwani wa mwaka 2010 walihakikisha wanakirudisha chama cha mapinduzi madarakani kwa kishindo. Kwani mkoani humo wapinzani waliambulia viti viwili tu tena vya udiwani.Kwa kweli hali hii inaudhi na inasikitisha sana. Natoa wito kwa Mh Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya M. Kikwete, chonde chonde Baba ondoa hii kero ni aibu kwa serikali yako.
3 comments :
Very good.
tujitahidi kudai maendeleo ya Tabora huko ndiko viongozi wengi wamesoma, nashindwa kuelewa ni kwa nini wamepasahau.
Uchangiaji nao una asili/tabia yake kwanza inabidi tuaanze kwenye familia kuaanda watu tangu wakiwa wadogo wajuwe kuwa kuna kujitolea kwenye jamii kwa ajili ya wengine.
Kassembo
Post a Comment