News
Loading...

Breaking news! Nyuki wazua kizaazaa katika mazishi ya aliyeuawa kwa kukatwa mapangaHapa tukikimbilia mayowe toka msibani.

Picha hii niliipiga nikiwa nimelala chini baada ya nyuki kuvamia.

MANUNDU; Hii ndiyo kazi ilifanywa na nyuki.

Kina mama wakijificha nyuki majanini.
Jioni hii majira ya saa kumi na nusu wakazi wa kijiji cha Itetemya, mkoani Tabora baada ya kuswalia maiti tukaelekea makaburini, tulipoanza kuzika tu tukaanza kusikia mayowe ya kina mama toka msibani ambapo pana urefu wa  kama mita 1000 hivi mpaka makaburini, ndipo baadhi yetu tukakimbilia kujua nini kimetokea huku wengine wakisema labda muuaji karudi na kuanza kushambulia watu wengine pale msibani. Tulipofika karibu na msibani tukaambiwa kumbe walikuwa nyuki wakimshambulia Mzee mmoja ambaye hata hivyo aliokolewa na wasamaria wema. Tukiwa hata hatujageuza kurudi makaburini nyuki wakatuvamia ikawa wenye kukimbia wenye kulala chini haya alimuradi kila mtu alijiokoa kivyake. Mtu mmoja alishambuliwa sana na nyuki ikawachukua wasamaria wema nusu saa kumuokoa, baadaye alipatiwa lifti ya gari ya Polisi kupelekwa Hospitali ya Kitete. Inasemekana hali yake ni mbaya sana baada ya kuumwa na nyuki wasiopungua mia. Watu wengine wanadai nyuki hao waliletwa kimazingara kwa kuwa aliyekufa alikuwa mtu mzito.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Anonymous said...

poleni!

Anonymous said...

hahahahahah!!! Jamani nakufa maana sina mbavu. Samahani sicheki kwa mazuri lahasha Isipokuwa manundu ya nyuki hahahaha!!!
Du Poleni sana ndugu zangu mkala pole.nyuki hatari sana.
Na Aliye kuwa Hospital Inshallah Mungu ata muhafu masikini.
A.M

Anonymous said...

Du!! HII NOMA.POLENI SANA
INASIKITISHA.