News
Loading...

Baada ya kuua kwa kutumia panga, Ajiua kwa kujinyonga!


Nyumbani kwa Bilali Kimwaga.
Kama mnakumbuka, juzi niliandika habari yenye kichwa Mauaji ya kinyama Itetemya, Tabora, mtuhumiwa wa mauaji yale ya Bi Asha Nyange Said kijana Bilali Kimwaga asubuhi ya leo amekutwa karibu na nyumbani kwao akining'inia mtini huku akiwa na kamba shingoni. Kwa haraka haraka inaonekana dhambi ya kuua ilimtesa kwa siku 3 hizo ambazo alikuwa akijificha maporini, na pia kutokuwa na pesa kumepelekea huyu kijana kujitoa uhai, kwani hakuweza kukimbia nje ya Tabora. Hata hivyo uchunguzi unaendelea ili kupata uhakika wa sababu ya kifo chake. Baba mdogo wa marehemu amethibitisha kuwa Bilali Kimwaga amejiua na mazishi yake yatafanyika leo jioni hapa hapo Itetemya.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :