News
Loading...

Mauaji ya kinyama Itetemya, Tabora.


Hii ndiyo nyumba ya familia ya Kimwaga Songoro.
Mkazi wa kijiji cha Itetemya Bi Asha (Nyange) Said (68) ameuawa kwa kukatwa katwa na panga jana majira ya saa 10 za jioni nyumbani kwake kilometa tano toka Tabora mjini. Akithibitisha tukio hilo askari wa kituo cha polisi Tabora mjini Bw Mhele Ngulati ameeleza kuwa mtuhumiwa wa mauaji hayo Bw Bilali Kimwaga (30) na familia yake wamekuwa wakimtuhumu marehemu kumroga na kumuua baba yao Bw Kimwaga Songoro baada ya kuwa na mvutano wa umiliki wa miembe iliyopo kati ya nyumba zao, mtuhumiwa hajakamatwa mpaka sasa. Bi Asha alikuwa ametembelewa na mjukuu wake wa kike kutoka mjini ambaye inasemekana alikimbia kujisalimisha baada ya kuona Bilali anamshambulia bibi yake kwa panga. Bi Asha anatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni haoa hapo Itetemya. Hata hivyo inashangaza ni vipi wagombee miembe au ardhi katika eneo hilo kwani ni eneo ilipo Ikulu ya Watemi wa Unyanyembe na wao au wazazi wao walikaribishwa hapo na Mtemi Saidi Fundikira baba wa marehemu Chief Abdalla Fundikira aliyetawala kuanzia mwaka 1917 mpaka 1927. Kisheria mahala hapo hapawezi kuwa na hati za umiliki nyingine ila ile ya Ikulu ya Unyanyembe tu. Eneo la Ikulu ya Unyanyembe lina ekari 432.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :