News
Loading...

Stop this media stunt!Mh Rais J.K. Kikwete.
Mwezi uliopita tumeshuhudia Rais Kikwete akitembelea wizara kadhaa kuona jinsi wanavyofanya kazi na kadhalika, kimtazamo alichokifanya Rais Kikwete ni kizuri lakini kuwafokea mawaziri wake live mbele ya kamera za televisheni sidhani kama ni jambo jema kufanya, mimi naona ni udhalilishaji wa hali ya juu. Kwani Mh Rais hana jinsi nyingine ya kuongea nao hata kama ameudhiwa na jambo fulani katika wizara husika? Hao mawaziri wana familia zao majumbani, hebu jiweke wewe katika nafasi ya mtoto wa waziri mmoja ambaye unashuhudia baba yako anavyoulizwa maswali kibabe namna ile utajisikiaje? Juzi Mkuu wa Mkoa wa Mara alienda kukagua shule za sekondari huko Tarime, akakuta shule moja ikiwa katika hali mbaya sana miaka miwili tu baada ya kujengwa huku sakafu za mabweni na madarasa zikiwa na mashimo makubwa humo ndani, Mkuu huyo wa mkoa alikasirika sana na kuanza kuiga mbinu ya Dk Kikwete kuuliza maswali kwa jinsi ya kudhalililsha kiasi kwamba alikaribia kumnasa vibao yule Mkurugenzi wa wilaya. Hii haikubaliki na nafikiri ni kinyume na haki za binadam. Zipo njia za wakuu hao kuwawajibisha watendaji wao si kuwadhalilisha katika runinga kisha wanawahamisha badala ya kuwafukuza kazi, yote hiyo ni kutaka kujikosha tu mbele ya wa Tanzania. Tumeistukia hiyo acheni mara moja tafadhali! 

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

5 comments :

Anonymous said...

angalia vibaraka wake wasije wakufuate wewe maana hawataki kuambiwa ukweli bado tunakuhutaji bwana kijana!

Mkala Fun said...

Nalielewa hilo lakini unapoamua kufanya kitu lazima ufikirie na kitakachoweza kutokea mbeleni, na mimi nimefanya hivyo. Vinginevyo nitausaliti moyo wangu nisipofanya ninayojisikia kufanya. Nashukuru kwa onyo mdau! Be strong!

Anonymous said...

Hilo neno Mdau,,kwani hawachelewi hao..ila ukweli always unauma.mhim democracy ikiwa kweli iko bongo usemaje wakowa ukweli itakulinda.MWENYEZI MUNGU BARIKI TANZANIA NAWATU WAKE PIA.Mdau IRELAND

Mzee wa Changamoto said...

Nakumbuka Martin Luther aliwahi kusema kuwa kama mtu anaogopa kusema UKWELI kwa kuwa anaogopa kuuawa, basi huyo HASTAHILI KUISHI.
Kwa maana nyingine, kama hujui WAJIBU ulioitiwa, ama unaujua na HUUTEKELEZI, basi hufai.
Ziweke hapa, la muhimu ni kuzima LABELS ili ziwe rahisi kutafutika. Kama nilivyofanya kwenye ka-baraza kangu mtoto ambapo KWA MFANO, ukitaka habari za Tanzania Yangu utaingia label yake (http://changamotoyetu.blogspot.com/search/label/Tanzania%20yangu), ukitaka kuona TUNAVYOIFIX SIASA waingia POLITICS FIX (http://changamotoyetu.blogspot.com/search/label/Politics%20fix) nk.
Kazi nzuri sana. Nimefurahi kuwa hapa

Mkala Fun said...

Thaks Mzee wa changamoto, notacheki blog zenu!