News
Loading...

Amin apita tena nomination za Kili Music Awards!Amin akikamua katika moja ya show.
Kwa mujibu wa orodha ya KILIMANJARO TANZANIA MUSIC WARDS Msanii wa muziki wa Bongo Flava Amin Mwinimkuu aka Amin amepita na kupendekezwa katika wawaniaji wa tunzo za Kili Music Awards za mwaka huu wa 2011, Amin ambaye nyimbo zake Ndo unikimbie na Yameteka dunia zinafanya vema katika vituo vya redio na vile vya runinga atakuwa amepata nafasi nyingine mwaka huu baada ya kuwemo pia mwaka jana na kuambulia patupu. Kwa vyovyote matumaini yake yamekuwa makubwa mwaka huu hasa baada ya kutikisa na wimbo wake wa Bado robo saa na baadae Ndo unikimbie. Mimi binafsi nampongeza Amin na namtaka asikate tamaa hata asipotwaa tunzo mwaka huu pia, azidi kujituma na ipo time atashinda. Kwa mwaka huu Amin anagombea tunzo ya wimbo bora wa Afro pop ambapo amewekwa yeye Amin na bado robo saa, swahiba wake Barnaba na kubembelezwa na wa ubani wake Linah akiingia na atatamani pia wamo Sam wa ukweli na sina raha Top C akiingia na wimbo wake Ulofa. Kazi ipo

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :