News
Loading...

UEFA wanacheza!


Kabali
Shirikisho la soka la Ulaya UEFA linaloongozwa na Michel Platini ambaye alikuwa mchezaji mahiri wa Les Blues timu ya taifa ya Ufaransa limeshangaza wengi baada ya kutoa adhabu ndogo na isiyostahili kwa mwanasoka mwehu wa klabu ya AC Milan Genaro Gatusso ya Italia. Gatusso amepewa adhabu hiyo ya kufungiwa kutocheza michezo minne baada ya kumkaba koo kocha Joe Jordan wa  Totenham Hotspurs ya England wakati mchezo ukiendelea na baada ya mchezo kwisha katika uwanja wa San Sirro jijini Milan, Italia. Hata hivyo Gatusso amekuwa mchezaji mshindani sana awapo uwanjani lakini katika mchezo huo wa kwanza dhidi ya Spurs ambapo Milan walifungwa goli moja kwa sufuri, Gatusso alivuka mstari kwani pamoja na kuwa wachezaji wa timu zote mbili kujaribu kumzuia bado aliendelea kufanya fujo uwanjani kwa muda usiopungua dakika tano hivi. Binafsi nilibaki kinywa wazi sikuamini kilichoendelea hapo na sasa siamini ambacho kimetokea jana kwa UEFA kumuadhibu kiduchu Gatusso aka animal (mnyama). Nimesoma gazeti the sun la kiingereza mwandishi Jim Munro kaenda mbali zaidi na kusema angekuwa mchezaji aliyefanya fujo anatokea katika vilabu vya England UEFA wangemtoa kafara kwa kumfungia mechi nyingi kama ilivyomtokea Didier Drogba alipofanya fujo kiduchu baada ya Chelsea kutolewa na Barcelona mwaka 2009 lakini akaangushiwa rungu la mechi sita na UEFA. Anyways tusisahau wale ni wataliani na klabu zao zilishapatikana na kashfa ya kununua na kuuza mechi so anything is possible with these lot. Ukweli utabaki kuwa Genaro Gatusso kapendelewa.
FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :