News
Loading...

HMbizo arudi kivingine!


Add caption
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava Hamisi Mbizo aka HMbizo ambaye alitamba na nyimbo kama Mchumba,Zuzu na Kunguru ametoa single mpya iitwayo Mvute mvute ambayo imetengenezwa na producer More Fire na tayari imeanza kukimbiza katika vituo kadhaa vya redio hapa jijini. Wimbo huo ambao unamzungumzia msichana ambaye yeye kavutiwa naye na anampenda lakini msichana huyo amekuwa akimringia na hivyo yeye kuamua kwenda kumtia ujinga kwa mganga Tawile. Hasa ukisilkiliza mashairi ya wimbo huo utacheka lazima kwa kuwa ni kisa cha kuchekesha kiaina. HMbizo anasema kuwa kwa sasa yeye na director wa video wanajipanga na kutengeneza script ili video ya wimbo huo ifanyike mapema wiki ijayo. Aliongeza'' Kesho nitakutana na director wa video ili tupange tunafanyaje ambapo natumai wiki ijayo tutaanza ku shoot mzigo. Nilipomuuliza ni kampuni gani anatarajia kufanya nayo video hiyo alijibu "Ah nafikiri hilo tuliweke pembeni kwanza, kisha tutafahamishana nani atakuwa amefanya mzigo huu" Kabla ya kuachia mvute mvute HMbizo alikuwa kimya kwa muda mrefu ambapo mwenyewe anadai alikuwa akiusoma mchezo, ambapo baada ya kuuelewa ndio amekuja kama hivi ambapo track hiyo inasumbua redioni. Na mimi nasema all the best kwake!
FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :