News
Loading...

WOLVES 2-1 MAN UNITED
Pamoja na Louis Nani kuifungia goli moja la mapema bado miti yote iliteleza huko Wolverhampton katika uwanja wa Molineux na kupeleka kilio Oldtraford. Wolverhampton wonderers timu iliyo chini kabisa ya msimamo wa ligi hiyo maarufu duniani English Premier League (EPL). Baada ya kuongoza kwa goli la Nani mnamo dakika ya 3 tu ya mchezo, Man united ilisalimu amri na kupoteza rekodi yake ya kutofungwa tangu Chelsea iliposhinda Oldtrafford mwezi wa nne mwaka 2010. Kevin Doyle aliifungia wolves goli la pili kwa kichwa baada ya Elokobi kuisawazishia timu hiyo inayofundisha kocha Mick McCarthy mnamo dakika ya 10 ya mchezo. Hadi timu zikienda mapumzikoni Wolves ilitoka kifua mbele kwa goli 2-1. Matokeo hayo yalibaki hivyo hadi firimbi ya mwisho ya mchezo.Man united ingeweweza kuepuka kipigo leo ingekuwa imevunja rekodi yake yenyewe ambapo ingekuwa haijafungwa katika michezo thelathini ya ligi hiyo ngumu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :