News
Loading...

Fagason akimbilia Extra Bongo!


Rapa mahiri wa Bendi ya Twanga Pepeta Paulo John aka Fagason na Rogart Hega (Catapiler) amejiunga na bendi ya Extra Bongo inayomilikiwa na Ally Choki, kuondoka kwa Fagason kumetokea baada wanamuziki Khalid Chokraa na Kalala Junior kuondoka na kwenda kaunzisha bendi yao ya mapacha watatu ambayo humjumuisha pia Josee Mara toka Fm Academia. Jinamizi hilo la kuondokewa na wanamuziki limewapitia pia na wacheza show Mahiri Nyamwela na Otilia. Matukio kama haya yamepata kuitokea bendi hiyo miaka ya nyuma pale nyota wake Ramadhani Massanja na Ally Choki walipoondoka na kujiunga na bendi za TOT na Extra Bongo kwa nyakati tofauti. wakati huo Extra Bongo ikianzishwa rasmi.Lakini Mkurugenzi wa ASET kampuni inayomiliki bendi hiyo aliwahi kusema kuwa bendi hiyo ni sawa na vilabu vya Simba na Yanga havitokufa kwa mchezaji mmoja kuondoka katika timu hizo.
Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya muziki wa dansi wameonyesha wasi wasi wao kwa kusema kuondoka kwa wanamuziki hao katika kipindi hiki ambacho bendi hiyo imekuwa ikifanya vizuri ni njama za wapinzani wao kuidhoofisha bendi hiyo ambayo kwa sasa ndiyo bendi inayoongoza kwa kuingiza wapenzi wengi katika maonesho yao kuanzia jumatano pale Club Billicanas, Alhamisi Club Sun Cirro iumaa Dar West Tabata, jumamosi pale Mango Garden aka Twanga City, jumapili Leaders Club mchana na TCC Club usiku.
Mr and Mrs Fagason.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :