News
Loading...

Kilabu cha mastarehe sun cirro jijini Dar.
Dogo Rama jukwaani Sun cirro.
Kilabu cha starehe Sun Cirro ni moja kati vilabu bora zaidi hapa nchini, jinsi ilivojengwa na umaliziwaji wake wa ndani ya kumbi hiyo ni wa daraja la kwanza. Ama kwa hakika unaweza kuuweka katika daraja moja na vilabu vingine maarufu jijini kama Club Maisha na club Billicanas. The African stars (Twanga pepeta) hutumbuiza hapo kila siku ya alhamisi.Kama ilivyo ada kwa bendi bora  Twanga  pepeta kipindi hiki, inajaza watu mno kwa kifupi panapendeza sana siku za alhamisi. Ukiitazama hiyo picha ya dogo Rama kulia kwake nyuma utaona boti la runinga ya mionzi (projector) runinga hilo huwashwa nyakati Bendi au hata muziki wa disko upigwapo. Lakini kwa maoni yangu runinga hilo labda lingekuwa linawashwa au lingehamishiwa pahala pengine humo ukumbini, nasema hivyo kwa kuwa alhamisi iliyopita runinga hilo liliokuwa likionesha filamu nzuri na ya kusisismua, na kwa kama dakika 10 hivi nilivutwa na kuanza kuifuatilia filamu ile akilini mwangu nisikumbuke kilichonipeleka pale ni kuwaona Twanga wakitumbuiza LIVE ON STAGE. Mara nikashtuka na kujisuta na kurudi tena kutazama burudani ya twanga, lakini sidhani kama runinga lile lisingekuwa pale pale wanapoimbia na kucheza Twanga ningeweza kuvutwa kirahisi vile. Nashauri tu wahusika walitoe au wasiliwashe wakati wa live shows ili tuweze kufuatilia kwa umakini kinachotupeleka pale Club Sun Cirro.Na yote hayo yametokea kukioneshwa filam, je ingekuwa Man United wanacheza dhid ya The Gunners?
Madansa wa Twanga ndani ya Twanga city.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :