News
Loading...

Matamshi yanapomshinda mtangazaji!


Hii ndiyo alama ya Barcelona Fc

Hii ni ni alama ya Mashetani wekundu.
Kuna baadhi ya watangazaji wa redio na runinga hunichosha kweli, unakuta mtangazaji mzoefu wa kipindi cha michezo anaitaja Barcelona kama BAKA, au utasikia Andy KOLE badala ya ANDY COLE  (KOL). Kama timu hiyo hutamkwa BASELONA kivipi kifupi chake kiwe BAKA badala ya BASA? Tena basi anayetamka hivyo ni mtu anayefuatilia ligi zote barani Ulaya hadi unastaajabu, inafikia mpaka wanapotosha uma wa washabiki wa soka. Au kingine na chenye kuudhi zaidi ni kuiita Man United MANI, yaani mtangazaji kakaa pale mbele anachambua mchezo kavaa suti kubwa lakini anaonea leo hii MANI watapanga kikosi cha kwanza. Mimi nawaomba wajirekebishe kwa kuwa wanapotosha watazamaji wao hasa wale wenzangu na mimi pangu pakavu.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :