Kolo Toure aponzwa na vidonge vya mkewe. |
Mlinzi wa kati wa klabu ya Manchester city na Ivory Coast Kolo Toure(29) amesimamishwa na kilabu chake kushiriki mazoezi na mechi za klabu hiyo na huenda akafungiwa kucheza soka kwa kipindi cha miaka miwili na taasisi ya kuzuia madawa ya kuongeza nguvu kwa wanamichezo World Anti Doping Agency (WADA).Toure alipimwa baada ya mchezo dhidi ya Man United uliofanyika Old Trafford pamoja na kuwa alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumiwa katika mchezo huo na baada ya vipimo alikutwa (positive) na chembe chembe zilizopigwa marufuku na (WADA). Akithibitisha hilo kutokea mmoja wa washauri wa Kolo Toure, Bwana Valere Gourison alisema "Ni kweli klabu yake imemsimamisha, nataraji kwenda England baada ya muda mfupi ili tukalijadili na klabu yake, kwa sasa wananisubiri ili tukae chini. Kolo amekuwa akitumia vidonge ambavyo mkewe alitumia kupunguza uzito naya amevitumia ili kupunguza uzito, kwa bahati mbaya vidonge hivyo vina kitu kinachokatazwa na (WADA) Tunatumai haitofikia hatua ya Kolo kufungiwa. Toure ambaye analipwa pauni 120,000 kwa wiki ameajikuta kuwa na msimu mbaya baada ya kuvuliwa unahodha nA locha Roberto Mancini na msimu huu ameshindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha klabu hiyo ya Eastland. Arsene Wenger alimnunua toka Asec Mimosas ya Ivory Coast na baadaye mwaka 2009 alimuuza kwa Man city kwa pauni 16 milioni. Hata hivyo Toure anaweza akaepuka adhabu hiyo iwapo kipimo cha pili (b sample) kitaonesha majibu mazuri kwake.
0 comments :
Post a Comment