News
Loading...

Harusi yavunjwa kisa bibi atafutiwa mchumba tajiri!


Kijana Najab ambaye leo hii usiku wa saa mbili alikuwa afunge ndoa na mchumba wake wa takriban miezi minne hivi amefanyiwa ukatili wa hali ya juu kwa ndoa hiyo kuvunjwa. 
Kijana Najab ambaye anafanya kazi katika kampuni ya kutengeneza maji ya samawati tulivu iliyopo Mikocheni Light Industry karibu na ITV, amekuwa akijiandaa na siku hiyo kubwa tangu mwishoni mwa mwaka jana ikiwa ni pamoja na kufanya matengenezo makubwa nyumbani kwake, kununua furnitures na vingine vingi tu. Leo hii mchana mimi na wenzangu kadhaa tulialikwa  karamu na Mama wa Najab aitwae Bhai Rukia katika kusheherekea ujio wa mke wa Najab. Tulipofika pale tukakuta wanaume watatu bila kujua nini kiliwaleta baada ya muda wakaondoka. Ndipo tukatanabahishwa kuwa wale waliotoka pale ni baba za mke mtarajiwa na wamekuja kwa mume mtarajiwa kukagua atakapoenda ishi binti yao, hii kali! Tukapuuzia mambo yale tukapata mlo kisha tukasambaa kwenda subiri muda wa kwenda kuoa ambao ulipangwa uwe saa 2 usiku katika msikiti Shadhiriya Kariakoo jijini Dar. Ilipotimu saa 1usiku ndipo wale mabwana watatu wakarudi na kusema kuwa wameonelea harusi iahirishwe mpaka Bw Najab atakapokaa vema kifedha nk, walipobanwa sana ndipo wakasema wameona hawawezi kumtoa binti wao aende akae hapo kwani hapana hadhi ya mtoto wao kuishi.Kama ilivyo ada penye wengi hapakosi neno, inesemekana mmoja wa wale mabwana watatu waliofika mahala pale ndiye mchumba mpya na inasemekana FLUSI ipo na ana biashara lukuki nchini China. Kwa hiyo hivyo huyo bi harusi amepigwa mnada na mwenye dau kubwa ndio kapewa. Pamoja na kudai wao ni waumini  wa dini ya ki Islam , sidhani kama Muslim yeyote angeweza kufanya kitendo cha kinyama kama hicho. Mungu atuweke mbali na watu kama hawa. Audhu Bilahi mina shaitanil rajim!
ndugu mdau kesho nitaweka picha za nyumba ya kijana Najab.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Anonymous said...

Du!! hii kali. Bi harusi kweli alikuwa na mapenzi ya kweli na Bwana Najabu? Mungu ata mpa kilicho na kheri kwake bwana Najabu Inshallah!!
A.m

Anonymous said...

nahuyo binti nae yumo katika mnada huo? Tahari ichukuliwe kabla ya uchumba kuingia hatua hii ya kuoa. Mwenyezi Mungu atampa kijana haki yake atapata mwenza kuliko huyo. Ni afadhali wamejionesha mapema, kijana kanusurika, wala asisikitike, bali ashukuru.

Anonymous said...

Kila mwanamke anataka kutunzwa!