News
Loading...

Xavi anapomuudhi Wenger


Arsene Wenger
Xavi Hernandes
Kiungo wa Fc Barcelona  Xavi Hernandes amemuudhi manager wa Arsenal Fc baada ya kukaririwa na vyombo vya habari akisema Cesc Fabregas anaumia na kuteseka moyoni kwa kuwa Arsenal hawataki kumuuza kwa Barcelona. Wenger anasema Xavi amekosa heshima na nidhamu kwa Arsenal na Cesc Fabregas mwenyewe kwa kutamka hilo kwa vyombo vya habari. Inaelekea wachezaji wa kihispania wana tatizo na nidhamu  kwani baada ya Spain kushinda kombe la dunia nchini South Africa kipa Pepe Reina alimvika Fabregas jezi ya Barcelona, sijui UEFA na FIFA wana mtazamo gani juu ya mambo kama haya ambayo ni sawa na kumshawishi mchezaji aliye chini ya mkataba na timu nyingine ajiunge na timu nyingine bi.lka kuishirikisha timu yake.

Kabla haya ya Xavi hayajaisha kocha wa Man City Roberto Mancini naye kaanza chokochoko kwa kuviambia vyombo vya habari kuwa anamtaka Samir Nasri pasi na kuongea na klabu husika yaani Arsenal. Nafikiri umefika wakati sasa FA,UEFA na FIFA kuwachukulia hatua watu wenye kuwa Unsetle wachezaji wa vilabu vingine.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :