Waziri wa ulinzi Kostas Papakostas na mkuu wake wa majeshi Patro Salkidis wamejiuzulu nyadhifa zao kufuatia mlipuko katika ghala la kuhifadhia silaha ambao ulisababisha vifo vya watu kumi na mbili, mlipuko huo mkubwa uliotokea kusini mwa nchi ya Cyprus juzi baada ya ghala la silaha kushika moto . Nguvu ya mlipuko iliathiri vibaya vijiji vya vya jirani na kukiharibu kinu cha kuzalishia umeme na hivyo kulifanya eneo kubwa la nchi hiyo ya Cyprus kukosa umeme.
Tofauti na Tanzania hata waziri akosee vipi kujiuzuru ni mwiko na kufukuzwa kazi ndio wala usfikirie kutatokea, inabidi tubalike jamani!
0 comments :
Post a Comment