News
Loading...

Kwa nini serikali inamtenga Chief Abdallah Fundikira linapokuja suala la uhuru wa Tanganyika?


Mtemi Abdallah Fundikira wa pili toka kushoto
na mwalimu Nyerere.
Tulipoadhimisha miaka 50 ya uhuru pale uwanja wa taifa na baadaye IKULU pakawa na utoaji wa nishani kwa wawakilishi wa walioshiriki kupigania uhuru. Pale yalitajwa majina 14 kwa mshangao wangu na wa ukoo mzima wa Fundikira hatukusikia jina la Chifu Abdallah Said Fundikira ambaye alitumika kuwashawishi machifu wenzie waiunge mkono TANU katika harakati za kugombea uhuru na alifanikiwa kuwashawishi na wakaiunga mkono TANU hatimaye kupata uhuru. Lakini tangu Mwalimu Nyerere alipoanzisha mfumo wa chama kimoja ndipo walipokorofishana na mpigania uhuru mwenzie Chifu Abdallah Fundikira ambapoa baadae walikubaliana kutokubaliana na ndipo Chifu Fundikira akajiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri wa sheria 1963. Lakini tangu siku hiyo serikali ya za TANU na baadaye CCM zimekuwa hazimtendei haki kiongozi huyo na si yeye tu hata babu wa babu yake Mtemi Isike Mwana Kiyungi amekuwa akiwekwa pembeni pale anapotajwa Mtemi wa Tabora na badala yake kutajwa Mtemi Mirambo pekee na hata ukiangalia majengo pacha ya benki kuu ya Tanzania yanaitwa Mirambo Towers. Sijapata kusikia hata uchochoro tu umepewa jina la Mtemi Isike. Kana kwamba hiyo haitoshi Chifu Abdallah Fundikira kapewa mtaa pale Magomeni Makuti, mtaa huo una nyumba zipatazo kumi tu ukifananisha na wapigania uhuru wengine. Sasa kwa nini hayo yanatokea mimi sielewi labda iulizwe serikali.

Mtemi Abdallah Fundikira wa kwanza kushoto
na Mwalimu Nyerere (suti nyeupe)
Mtemi Said Fundikira baba wa Mtemi Abdallah Fundikira akiwa na
mwalimu Nyerere enzi hizo 1956.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

3 comments :

Subi said...

Asante kwa historia fupi. Ama kwa hakika suala hili na yanayowahusu viongozi waengine wapigania uhuru, ukombozi na maendeleo ya Tanzania, anayeweza kutoa sababu hasa ya kwanini wengine wakumbukwe na wengine wasahauliwe kwa makusudi ni Serikali na uongozi wake.

Uzuri ni kuwa uhuru wa kuweka kumbukumbu kwa watu binafsi ungali bado upo na huenda kwa kuziandika hivi, siku moja zitatambulika rasmi na wahusika kupewa heshima zao ikiwa wanazistahili.

tz biashara said...

Historia yenyewe tuliyofundishwa mashuleni haikuwa yaukweli na yale ya ukweli yamefichwa kwa sababu ya kupewa kipaumbele mtu mmoja tu.Waliohangaikia uhuru kwa hali na mali hawafahamiki isipokuwa wale waliokabidhiwa uongozi kiulaini bila kutoa jasho kama wenziwao ndio wanaonekana.Sio Chifu Fundikira tu bali wengi wanaopaswa kukumbukwa.

tz biashara said...

Wapo wengi tu waliosahaulika kwa makusudi ili kumtukuza mtu mmoja tu.Wapo waliopigania kwa hali na mali kujitolea kwa kutafuta uhuru na matokeo yake tunafundishwa sivo mashuleni ktk historia.