News
Loading...

Congo yalaumiwa kwa kutolinda watoto lakini Tanzania nayo imo!


Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 wakifanya kazi katika migodi nchini Congo DRC.
Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane wamekuwa wakifanyishwa kazi migodini. ili kuwawezesha kukidhi mahitaji yao pamoja na familia kutokana na umaskini.Mashirika ya kutetea haki za watoto yanailaumu serekali ya nchi hio kwa kutochukua hatua madhubuti dhidi ya kampuni za uchimbaji madini zinazoajiri watoto.
Lakini huku jumuiya za kimataifa zikiilaumu Congo DRC nchi nyingi za kiafrika zina tatizo la kutolinda watoto ikiwemo nchi yangu pendwa ya Tanzania, mwezi desemba nilikwenda Singida kwa shughuli za kikazi nazo zikanifikisha katika kijiji kidogo cha Kipuma ambako tulikuta watoto wadogo chini ya miaka 18 wakifanya kazi katika mgodi mdogo wa Kipuma ambako panapatikana madini aina ya Zircone. Hivyo basi hii ni dhahiri kuwa tatizo hili lipo hata nchini kwetu Tanzania. Cha msingi ni serikali kuangalia jinsi ya kusaidia familia hizi duni ili ziondokane na tatizo hili la watoto kufanya kazi badala ya kwenda shule.
Huu ni mgodi mdogo wa Kipuma, Singida ambako nilipiga picha hii.
Kipuma Singida. Mtoto huyu tulimkuta akichimba na alishapata madini mawili aina ya zircone ambayo alituonesha.
Hali hii ni kawaida katika nchi ya Congo Drc.

Habari na picha kwa ushirikiano wa keronyingi blog na BBC Swahili

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :