News
Loading...

Serikali ya wanafunzi IFM yakanusha kumpigia chapuo Lowassa uRais 2015


Serikali ya wanafunzi chuo cha usimamizi wa fedha IFMSO kupitia msemaji wake mkuu rais wa serikali hiyo imekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la NIPASHE la tarehe 19/2/2015 lililokuwa na kichwa cha habari WANAFUNZI IFM WAMTAKA LOWASSA URAIS na kuwa taarifa hizo hazikutolewa na serikali ya wanafunzi IFMSO wala hakuna mkutano wowote uliofanyika katika maeneo ya chuo hicho kilichpo katikati ya jiji la Dar es Salaam kati ya waandishi wa habari na uongozi wa wanafunzi wa chuo hicho na kuweka bayana kuwa wao wanamtaka LOWASSA awe Rais katika uchaguzi ujao. Pia kulingana na katiba ya IFMSO kifungu namba 3 ibara ndogo ya kwanza, inakataza wanafunzi (IFMSO) kushiriki katika masuala yeyote ya kidini na kisiasa hivyo basi IFMSO imesikitishwa na taarifa hiyo potofu na inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na taarifa hiyo.

Imetolewa na Clonton Boniface
Rais wa serikali ya wanafunzi IFMSO 19/02/2015

Habari kwa hisani ya Michuzi Blog

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :