News
Loading...

Hukumu ya Swetu Fundikira ni fundisho kwa askari wote Tanzania


Kutoka kulia Sajenti Rhoda Robert (45), Koplo Ally Ngumbe (40) na Rashid Ally (30) wakisubiri kusomewa hukumu jana.
Baada ya kesi ya mauaji ya Swetu Fundikira kufikia tamati jana kwa watuhumiwa ambao ni askari jeshi Sajenti Rhoda Robert (45), Koplo Ally Ngumbe (40) na Rashid Ally (30) kupatika na hatia ya kumuua kwa makusudi Swetu, Mh Jaji Zainab Mruke wa Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam aliwahukumu washtakiwa hao kunyongwa mpaka kufa. Hukumu hii inatoa fundisho kubwa kwa baadhi ya askari jeshi na polisi na hata wale wenye madaraka serikalini kuwa hawapo juu ya sheria, kwani tumeshuhudia tukio la Ditopile wa Mzuzuri na lile la hivi karibuni ambapo askari wa kutuliza ghasia alipomuelekezea na kumfyatulia bomu la machozi mwandishi wa habari David Mwangosi na kumfumua tumbo na kifua na kupelekea kifo chake katika tukio lililojiri huko mkoani Iringa.Kumekuwa na matukio ya askari wa kutuliza ghasia kutumia nguvu kubwa sana katika kuzima ama maandamano au mikusanyiko na matokeo yake kupelekea kujeruhi au kukatisha maisha ya watu jambo ambalo ni kinyume na haki za binadamu. Sina shaka hata chembe kuwa David Mwangosi atapata haki yake, lakini Mungu hatoturudishia mwandishi huyo shupavu hivyo basi familia yake kuteseka kwa kumkosa kuwaongoza katika maisha yao ya kila siku.

Mkae mkijua sasa hakuna pa kujifichia mkitenda maovu sheria itafuata mkondo wake, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :