Kipande cha makala hiyo kikionesha picha ya Sheikh Ponda na wasichana waliojeruhiwa kwa tindikali mjini Zanzibar.
Jeraha la Sheikh Ponda
Sheikh Ponda akiwa hospitalini Muhimbili.
Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeandika kupitia mtandao wake www.mailonline.co.uk habari kuwa Sheikh Ponda anahusishwa na shambulio la tindikali dhidi ya wafanyakazi wa kujitolea (volunteeres) raia wa Kiingereza Katie Gee na Kirstie Trupwote wenye umri wa miaka 18 ambao siku chache zilizopita walipatwa na mtafaruku wa kumwagiwa tindikali ambapo wamepata majeraha makubwa kutokana na shambulio hilo. Mtandao huo pia umeeleza kuwa Sheikh Ponda alijeruhiwa kwa risasi ya bomu la machozi jana baada ya kujaribu kuwatoroka polisi ambao walikuwa wamekwenda kumkamata kwa tuhuma juu ya shambulizi la tindikali. Hizi ni picha za Sheikh Ponda akiwa hospitali ya Taifa Muhimbili.
Picha za Sheikh Ponda na Habari kwa hisani ya KapipiJBlog
0 comments :
Post a Comment