News
Loading...

Mtoto wa miezi 8 achomwa kwa mkasi mara 90 usoni na mama yake mzazi kisa alimuuma alipokuwa akimnyonyesha!


Mtoto Xiao Bao (miezi 8) amejeruhiwa vibaya na mama yake mzazi baada ya Xiao kumuuma mama yake alipokuwa akimnyonyesha. Xiao Bao ambaye kwa sasa yupo hospitalini akiuguza majeraha ya mkasi na nyuzi( Stitches) zaidi ya 100 nyingi ya hizo ni usoni. Xiao Bao aliokotwa na mjomba wake akiwa amelala katika dimbwi la damu nakupelekwa hospitali, mtoto huyo amekuwa akiishi na mama yake na wajomba zake wawili wanaofanya biashara ya kuuza taka zinazotumika kutengenezewa upya bidhaa mbali mbali katika jimbo la Xozhou, katika jimbo la Jiangsu. Inasemekana kuwa mama wa mtoto huyo baadae aliungama kuwa yeye ndiye aliyemjeruhi mwanaye baada ya kumuuma. Habari zaidi zinaeleza mamlaka mjini hapo ilisema hakuna uthibitisho kuwa mama wa mtoto huyo anasumbuliwa na ugonjwa wa akili. Hata hivyo majirani waliitaka mamlaka imchukue mtoto huyo toka mikononi mwa mama yake.


Mtoto Xiao Bao akiwa hospitalini
Tatizo la ugonjwa wa akili limeendelea kuwa kitu cha siri mno nchini China kwa sasa, kwani gonjwa hilo halitibiwi kisasa nchini humo. Mwaka 2009 jarida la kitabibu la Kiingereza The lancet lilifanya tafiti katika majimbo manne nchini humo na kugundua kuwa asilimia 90 ya watu wazima kati ya watu milioni 173 nchini humo wna tatizo la ugonjwa wa akili lakini hwajawahi kupata tiba yeyote ya ki taaalamu.

Habari na picha kwa hisani ya Mirror

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :