News
Loading...

Umoja wa Ulaya, UN; Tutapigania Uhuru wa Habari Siku Zote


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.

Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimio hayo. Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimisho hayo.Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani. Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu akifuatilia mijadala katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu akifuatilia mijadala katika mkutano huo.Mwanahabari na Bloga, Majid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo..Mwanahabari na Bloga, Majid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza. Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza.

Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.

Na Joachim Mushi, Morogoro 
Umoja wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya kikatili na unyanyasaji wameokuwa wakifanyiwa na vyombo vya dola vya Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari. Akizungumza leo mjini Morogoro katika Maadhimisho ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Kiongozi Mkuu wa Mabalozi hao, Balozi Filiberto Cerianse Bregondi alisema EU itaendelea kupinga namna yoyote ya unyanyasaji kwa wanahabari makundi yote wakiwemo wa mitandao ya kijamii hadi utakapo kuwepo uhuru kamili wa vyombo vya habari. "...Tulifanya hivyo kwa mauaji yalipotokea na tutaendelea kufanya hivyo siku zote watakapo kamatwa na kupigwa wakiwa kazini...Tunajua huenda haitoshi lakini hii ni kutokana na tofauti mbalimbali za kiutendaji," alisema Balozi Cerianse Bregondi. Alisema kupinga unyanyasaji kwa wanahabari haina maana wanachoandika wanahabari mara zote ni cha kweli lakini ipo namna nzuri ya kushughulikia mvutano kama huo na kusaidia kupata taarifa za kina zaidi zitakazofikia muafaka. Aidha kwa upande wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alisema Tanzania inaongoza Afrika kwa kushindwa kuweka utaratibu mzuri wa udhibiti mawasiliano. Alisema vyombo vya habari ni muhimu katika taifa na hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Taifa unaotarajia kufanyika Oktoba, alisema vyombo vya habari vinaweza kubomoa au kujenga taifa lolote. "...Waandishi ni watu muhimu katika kudumisha demokrasia nchini hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kujifunza zaidi. Maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kitaifa yamefanyika mkoani Morogoro na kuhudhuriwa na wanahabari mbalimbali, wakongwe, wadau anuai wa vyombo vya habari huku yakiwa na kauli mbiu ya Usalama wa Vyombo vya Habari katika Dijitali: Uhandishi Mzuri unaozingatia, Usawa wa Kijinsia na faragha.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :