Picha hii inaonesha jinsi maji ya mvua yalivyotengeneza mkondo barabarani huku mfereji wa maji ukionekana pembeni kulia ma barabara. |
Pichani juu ni kipande cha barabara ya Kilimatinde iliyopo Cheyo Tabora kinachoonesha jinsi ya ujenzi wa barabara usio makini kiasi cha kupelekea maji ya mvua kutengeneza mkondo katikati ya barabara huku mifereji iliyopo katika barabara ikiwa haitumiki na maji ya mvua. Na zimetumika pesa kujenga mifereji hiyo lakini ipo kama urembo katika eneo hilo.
Bila shaka wahusika washaliona tatizo hili na watalifanyia kazi kwa kutengeneza mwinuko katikati ya barabara yenye kutiririsha maji mferejini badala ya maji kupita barabarani.
Maghorofa ya National housing yakionekana kushoto mwa barabara hiyo ielekeayo Isevya kupitia chuo cha Reli Cheyo |
Kushoto ni moja ya mifereji iliyopo pembezoni mwa barabara hiyo ya Kilimatinde iliyopo karibu na maghorofa ya National Housing na Tanesco maeneo ya Cheyo. |
Mmoja wa baahi ya watumiaji wa barabara hiyo wakipunguza mwendo eneo lililo na mfereji barabarani |
0 comments :
Post a Comment