News
Loading...

Jack Wilshere azua zogo!


Mo Farah akishangilia baada ya kuishindia medali 3 Uingereza ingawa ni mzawa wa Somalia.
Mcheza soka mahiri wa kilabu cha Arsenal Jack Wilshere amezua zogo huko England baada ya kudai ni wenye utaifa wa Uingereza ndio wana haki ya kuichezea timu ya taifa ya Uingereza, ikielekea kuwa alisema hivyo baada ya Kocha wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson kusema angependa Adan Januzaj chipukizi wa Man United aichezee timu hiyo. Zogo hilo lilichukua muelekeo mwingine baada ya Kevin Pietersen aliyekuwa nahodha wa timu ya Cricket ya England ambaye ni mzaliwa wa South Africa kumuuliza Wilshere kupitia mtandao wa Twitter kuwa "wageni unaowamaanisha ni pamoja na mimi, Mo Farah? Pia Pietersen aliwataja mashujaa wengine walioineemesha England huku wakiwa si wazaliwa wa England. Jisomee mwenyewe majibizano kati ya Pietersen na Wilshere.
Pamoja na kubanwa na maswali ya Pietersen hivyo Jack Wilshere anaelekea kupata sapoti toka kwa kocha wake Arsene Wenger aliyedai kuwa itafikia nchi zitanunua wachezaji kama vilabu hali hiyo isipozuiliwa mapema. Lakini Ukweli unabaki kuwa nchi kama France ilishinda ubingwa wa dunia 1998 na wa Ulaya mwaka 2000 ikiwa na wachezaji zaidi ya watano akiwemo Marcel Dessaily, Lilian Thuram, Zinedine Zidane, na Patrick Vieira kwa kutaja wachache na wote hawa hawakuzaliwa France, je hali hii inatueleza nini?

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :