News
Loading...

Emmanuel Frimpong kiungo chipukizi wa Arsenal azua mjadala mtandaoni


Mchezaji wa kiungo chipukizi wa Arsenal Emmanuel Frimpong amezua mjadala katika mtandao wa TWITTER baada ya kudai angekuwa na nafasi kubwa ya kucheza Arsenal angekuwa mweupe na Mwingereza.

Frimpong akiwa mazoezini Arsenal

Frimpong aliulizwa katika mtandao wa Twitter kwa nini hayumo katika kikosi cha Arsenal ambacho leo usiku kitapambana na Chelsea katika mchezo wa kombe la Capital One alijibu kama ifutavyo "Lol I wanna laugh" Sometimes i wish i was English and white realtalk. Na mara Frimpong (21) akafuta twitt yake hiyo haraka sana, kisha akaandika nyingine ikisema " Look what ever you read tomorrow is majorly been twisted. Is a joke what people will do to start controversy goodnight people" alimaliza. 

Hata hivyo Frimpong si mgeni katika utatanishi, mwaka 2012 alipigwa faini na chama cha soka FA baada ya kutoa maneno ya kitata dhidi ya mshabiki wa Totenham Hotpurs. Amepata kuichezea Arsenal mara 6 tu na amekuwa akipelekwa kwa mkopo katika timu za Wolves, Chalton and Fulham.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :