News
Loading...

Kwa nini Kigwangallah ahangaike na sahihi za wabunge ili kumuondoa Spika Anne Makinda?


Nimesoma katika gazeti la Mwananchi la leo kupitia mtandao, humo nimekutana na makala isemayo "Hoja ya kumng'oa Spika Makinda yapigwa kombora"

Spika wa bunge la Tanzania Bi Anne Makinda

Mbunge wa Nzega kupitia CCM Bw Hamisi Kigwangwallah amekuwa akiendesha kampeni ya kumuondosha Spika wa Bunge katika kiti hicho baada ya kumtuhumu Spika kuwa alikiuka kanununi kwa kumteua Andrwe Chenge kuwa Mwenyekiti wa kamati ya bajeti badala ya kuchaguliwa kwa kura kama ilivyo kawaida pia Makinda amekiuka kanuni kwa kuidhinisha malipo ya Sh 430,000 kama posho kwa wajumbe wa kamati ya bajeti, tofauti na na wajumbe wa kamati nyingine ambao hupokea sh 180,000 kama posho kwa siku. Kinachonishangaza ni je? hakuna sheria nyingine zinazoweza kumbana Spika kwa uvunjifu wa kanuni hizo ili awajibishwe? kama ambavyo watumishi wengine wanavyoweza kuwajibishwa kwa kosa kama hilo? badala ya Kigwangwallah kutegemea sahihi za wabunge wengine wa CCM ambao wana fikra za kulinda maslahi ya chama chao tu? Natumai zipo njia nyingine ambazo Kigwangwallah anapaswa atumie kupitisha hoja yake.


FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :