News
Loading...

Breaking news! Kikombe kipya Tabora!


Huyu  ni dada Asha Baraka (35) anadai kuota kupewa uwezo wa kutibu magonjwa sugu.
Mimi nikiwa na Asha Baraka baada ya kumhoji.

Dawa ishachemshwa tayari kupewa wahitaji kuinywa.

Vikombe vipya, maalum kugawia dawa.

Hapa ndipo alipopanga Bi Asha Baraka

Mama huyu kutoka Urambo akisubiri kikombe cha dawa toka kwa Asha.
Mpendwa mdau pichani juu ni Asha Baraka(35) mkazi wa Mtaa wa Kakola, Kata ya Kanyenye mjini Tabora ambaye anadai siku ya alhamisi kumkia ijumaa tarehe 1/03/2011 ameoteshwa na Mwenyezi Mungu kutibu magonjwa yote sugu na atibu watu wa dini zote. Asha ambaye ni muumini wa dini ya ki Islam anasema ameelekezwa atumie majani ya mhindi kama dawa yake, achemshe ndipo awape watu wenye magonjwa mbali mbali. Na sikupoteza muda nikauliza watu kadhaa katika nyumba anayokaa Asha kama wametumia dawa hiyo na nikapata wawili wakidai tangu wanywe dawa hiyo wamepata nafuu ya maumivu ya mgongo na mwingine kiuno na na miguu. Awali Asha alikataliwa kugawia dawa katika nyumba aliyopanga ndipo akapewa nafasi katika nyumba jirani ambako ndipo alipanga kugawia dawa hiyo leo hii jioni. Mpaka nikiondoka hapo alikuwa hajaanza kugawa kikombe.

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :