News
Loading...

Marekani haijajifunza Iraq na Libya?


Rais wa Marekani Barack Obama

Tumeshuhudia jinsi nchi ya Libya ikipoteza muelekeo mara baada ya Muammar Gaddafi kukamatwa na hatimaye kuuawa. Pamoja na kuwa nchi nyingi za magharibi zilivalia njuga na kusaidia waasi walijiita wa wakombozi wa nchi ya Libya toka mikononi mwa Dikteta Muammar Gaddafi na familia yake. Lakini inadhihirika sasa kuwa tangu Gaddafi auawe nchi hiyo si tu imepoteza muelekeo tu bali pia amani imepotea kabisa na huwezi kufananisha na wakati  nchi hiyo tajiri wa mafuta ilipokuwa ikiongozwa na Dikteta Gaddafi,ambapo wananchi wa nchi hiyo waliishi kwa raha sana pamoja na serikali yao kuwajali walipotaka kuoa, kununua gari au nyumba nk. Serikali hiyo
Kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi
iliwachangia wananchi wake nusu ya kile walichotaka kununua
. Lakini leo wananchi wa nchi hiyo wanaishi maisha ya taabu. Pia hayo tumeyashuhudia Iraq ambapo ilielezwa na mataifa ya Magharibi hususan Amerika na England kuwa Dikteta Saddam Hussein aliua wananchi wake bila huruma, alitesa watu mbali mbali na kubwa zaidi tukaambiwa ana silaha za maangamizi ya halaiki ambazo atazitumia dhidi ya Israel na mataifa ya Magharibi na hivyo ilikuwa lazima aondoshwe madarakani na ashtakiwe kwa ukatili dhidi ya ubinadam. Marekani ikapata lake, Saddam akakamatwa na hatimaye kunyongwa. Lakini tangu hapo nchi hiyo imepoteza muelekeo kiuchumi na kila kitu

Rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein
Na  sasa tunashudia machafuko yanaoendelea nchini Misri, nchi hiyo imepoteza kabisa muelekeo mara baada ya jeshi la nchi hiyo kumuondosha madarakani Rais Mohamed Morsi wa chama cha Muslim Brotherhood ambaye alishinda uchaguzi huru na wa haki uliofanyika miezi kadhaa iliyopita. Na haielekei Marekani itachukua hatua kubwa zaidi ya kusimamisha misaada na uuzaji wa silaha kwa nchi hiyo. Labda tu niseme umefika sasa wakati Marekani na mataifa ya magharibi waache kuingilia mambo ya nchi nyingine na hasa mashariki ya kati ambapo wamefanikiwa kuzivuruga vya kutosha na kuziacha zikiwa na vita za wenyewe kwa wenyewe. Kwani hatuoni nchi hizo ambazo zilisemekana kukombolewa na Marekani zimefaidika nini tangu kuondoshwa kwa Saddam Hussein na Muammar Gaddafi

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :