News
Loading...

Hongera uongozi wa Simba sports club


Swedi Mkwabi Kiongozi wa kamati ya ligi akiwa na Kocha wa zamani wa Simba Sports Pat Liewig
Kitendo cha uongozi wa Simba Sports Club cha kumrudisha kocha mzawa Abdallah Kibaden King na kuwaondoa baadhi ya wachezaji nguli wa timu hiyo wakiwemo Haruna Moshi, Juma Nyosso na Juma Kaseja ni cha kishujaa mno, na ushujaaa huo umeanza kuonesha matunda baada ya timu hiyo yenye wachezaji chipukizi lukuki lakini wenye vipaji vikubwa kutoa sare ya kuvunja rekodi baada ya kuongozwa kwa magoli 3-0 mpaka mnamo dakika ya 55 hivi. Ambapo dakika chache nyuma waliingiza wachezaji chipukizi wawili wa kiungo Hamis Ndemla na William Gallas mabadiliko ambayo yaliisaidia zaidi Simba ambapo waliweza kurudisha goli zote 3 walizofungwa kipindi cha kwanza na kuufanya mcheza kuisha sare ya goli 3-3. Baada ya pongezi zangu kwa uongozi wa Simba napenda niwakumbushe kama wanapitiwa, pamoja na kuwa kipa wa timu ya Taifa ya Uganda The cranes, bado nahisi Abel Dhaira ndiye weakest link katka timu hiyo, kila atokeapo mipira ya juu ambayo ungefikiri ndio rahisi kwake kuicheza lakini hapana amekuwa hana hakika na nini aende akafanye pale, cha msingi kipa Juma Kaseja bado ni pengo la dhahiri. Hivyo basi naushauri uongozi huo wasije wakawa kama Marcio Maximo aliyemkataa Kaseja huku akiwa hana mbadala wake matokeo yake waTanzania 45m tukateseka kwa ujivuni wake dhidi ya Kaseja ambapo tulitolewa kirahisi katika mashindano yote tuliyocheza chini ya Maximo Huku akitumia makipa zaidi ya watatu bila mafanikio, makipa hao Ivor Mapunda, Mwadini Ally, Muharami Ally na hata msaidizi wa Juma Kaseja katika timu ya Simba, Ally Barthez

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala Fundikira

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :