News
Loading...

Mfa maji haishi kutapa tapa


Mshtakiwa wa pili Ally Ngumbe akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa. 
Baada ya Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam
kuwakuta wanajeshi watatu na hatia ya kumuua kwa makusudi Bw Swetu Fundikira (47) Mh Jaji Zainabu Mruke aliwahukumu watuhumiwa hao Sajini Rhoda Robert (45) koplo Ally Ngumbe (40) na nduguye Mohamed Rashid (30) kunyongwa hadi kufa. Bila kupoteza muda wakili wao wa utetezi Bw Mluge alisema anatarajia kukata rufaa kwa kile alichokiita kutoridhishwa na hukumu iliyotolewa mahakamani hapo.Alihoji ni vipi wateja wake wapewe hukumu hiyo huku kukiwa hakuna shahidi yeyote aliyeshuhudia washtakiwa wakimuua Marehemu Swetu Fundikira. Pili ni kuwa hata hayo majeraha ya kichwani aliyokutwa nayo marehemu ambayo yanaelezwa ndio chanzo cha kifo chake hayakutolewa maelezo yalipatikana vipi kwa kupigwa ama kwa jinsi gani.

Safari ya gerezani ikianza rasmi

Mimi si mwanasheria lakini napenda kuchukua nafasi hii kunukuu maelezo ya Mh Jaji Mruke kabla hajatoa hukumu, maelezo hayo yatajibu maswali ya wakili msomi Mluge. Akisoma hukumu hiyo Mh jaji Mruke alisema;

"Ingawa hakuna hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa washtakiwa hao ndio waliomuua Fundikira, ushahidi uliotolewa na upande wa Mashtaka ulikuwa ni ushahidi wa kimazingira na kwamba Jamhuri imeweza kuthibitisha mashtaka hayo. Alisema kuwa anakubaliana na mtiririko wa ushahidi wa upande wa mashtaka kama ulivyoelezwa wake sita akiwamo Daktari aliyeufanyia uchunguzi mwili wa marehemu Swetu Fundikira pamoja na askari polisi wawili ambao washtakiwa katika utetezi wao walishindwa kuuvunja.
"Sheria ipo wazi, ukiondoka na mtu au ukionekana naye kwa mara ya mwisho na baadaye mtu huyo akapatikana na madhara, wewe ndiye utkayewajibika kutoa maelezo ya kina ya juu ya yaliyomsibu mtu huyo" Alisema Mh jaji Mruke na kuongeza " Kisheria ukitoa maelezo ambayo hayakidhi haja na yenye utata ni faida kwa upande wa mashtaka ambao hutegemea ushahidi wa kimazingira. Maelezo ya kina hayakutolewa na washtakiwa wote"
"Ushahidi wa mashtaka japokuwa ni wa mazingira lakini umejengwa thabiti na upande wa utetezi umeshindwa kujenga matundu ama kuuvunja mnyororo huo, hivyo kidole kimewaelekea wao"

"Hivyo kosa wanaloshtakiwa nalo limethibitishwa na Mahakama imewaona washtakiwa kuwa wan hatia ya kumuua Swetu Fundikira"

FACEBOOK COMMENT

Share on Google Plus

Connect Mkala26

Usikubali kupitwa na chochote kupitia mtandao huu, kupaya yote haya unahaki ya kuungana nasi sasa, Kuungana nasi BOFYA
FACEBOOK, |INSTAGRAM,
.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :